Wafajasiriamali wadogo, makarani, pamoja na wabeba mizigo wa kituo cha Mabasi cha Magufuli, (Magufuli Bus Terminal) kwa kushirikiana na vikundi mbalimbali vya michezo, wadau wa mazingira na SUMA JKT wamemuenzi aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Joseph Magufuli kwa kufanya usafi kituoni hapo leo Machi 19,2022.
Katika usafi huo uliosimamiwa na watumishi wa Mazingira wa Manispaa ya Ubungo wajasiriamali hao wameahidi kuwa usafi utakuwa ni endelevu yaani utafinyika kila siku ya jumamosi ili kuendelea kutunza mazingira ya kituo hicho kikuu cha Mabasi cha Magufuli.
Aidha wajasiriamali, makarani na wabeba mizigo hao wameipongeza Serikali kwa kuwajengea kituo hicho na kwamba wameahidi kukitunza kwa kuhakikisha kinakuwa safi muda wote.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa