Wafanyabiashara wa kusaga unga Kata ya Manzese Manispaa ya Ubungo kwa hiari wamekubali kuanza kulipa ushuru wa kushusha na kupakia kulingana na uzito wa gari baada ya kukaa kikao na kukubalina na uongozi wa Manispaa hiyo.
Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kuwasilisha kwenye kikao hicho mapendekezo ya kuanza kutoza ushuru wa kushusha na kupakia ambapo wafanyabiashara wameishuruku Manispaa kwa kuweka kikao hicho kilichotoa fursa ya kutoa maoni yao kwani wangeweza kutekeleza sheria hiyo bila kutushirikisha.
Akiwasilisha mapendekezo ya ushuru huo, Mweka Hazina wa Manispaa Ndg. George Mzeru amewaeleza wafanayabiashara hao kuwa, Halmashauri imeona vyema kukutana na wafanyabiasha wa mashine za kusaga unga ili kujadili na kukubaliana kwa pamoja viwango rafiki vya kutoza kwenye chanzo hicho ili kila mfanyabiashara alipe badala ya kukwepa.
Baada ya majadiliano ya kikao hicho, wafanyabiashara wamekubali kulipia ushuru huo kwa siku, mwezi na mwaka ambapo kwa siku gari ya tani 2 hadi 3.5 itatozwa shilingi 5000, kwa mwezi 20,000 na kwa mwaka 300,000, kwa gari lenye uzito wa tani Zaidi ya 3.5 mpaka 10 kwa siku 10,000, kwa mwezi 50,000 na kwa mwaka 500,000 huku gari ya Zaidi ya tani 10 itatozwa shilingi 15,000 kwa siku, shilingi 70,000 kwa mwezi na shilingi 700,000 mwaka
“Uhuru wa kushusha na kupakia upo kwa mujibu wa sheriandogo za manispaa, halmashauri ingeweza kutekeleza sheria hiyo bila kuwashirikisha lakini kwa ajili ya kuboresha mahusiano na kujenga ukaribu na wafanyabiashara tumeona tukubaliane viwango rafiki ambavyo kila mfanyabiashara atalipa kwa hiari na bila kumuumiza” alifafanua Mzeru
Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara wanaosaga na kuuza unga Oscar Munisi ameipongeza halmashauri kwa kuitisha kikao hicho ambacho kimewapa fursa ya kutoa mapendekezo na kukubaliwa na Manispaa “ hii ni heshima kubwa kwetu na tunaahidi kulipa ushuru huu wa kushusha na kupakia bila kikwazo kwani viwango hivi ni rafiki”
Aidha, Mwenyekiti huyo amesisitiza Manispaa kuendelea kutoa elimu kwa wafanyabaishara juu ya tozo,ada, ushuru na kodi mbalimbali za halmashauri ili kujenga uelewa na utayari wa kulipa kwa hiari kwani mfanyabiashara akielimishwa vizuri hakatai kulipa kodi ya serikali.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa