Kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliotokea Nchi jirani ya Uganda Manispaa ya Ubungo imekutana na waganga wafawidhi wa vituo vya Serikali na binafsi pamoja na wataalam wa tiba za asili lengo ikiwa ni kuona utayari kwenye vituo vyao na jamii namna ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.
Wataalamu hao wameelekezwa namna ya kumtambua mshukiwa wa ugonjwa wa Ebola na wametakiwa kuwa na sehemu maalum ya washukiwa wa ugonjwa huo, kuboresha namna ya kujikinga na Ebola na wameelezwa namna ya kujikinga na ugonjwa huo.
Akiongea Dkt Felista Kimolo Mratibu wa huduma za dharura na majanga Manispaa ya Ubungo ameeleza kuwa Ebola ni ugonjwa hatari na tayari umeshatokea Nchi jirani ya Uganda hivyo ni vyema kuweka mikakati ya kujikinga dhidi ya Ugonjwa huo hatari.
Nae mganga mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt Peter Nsanya amewataka wataalamu wao kuhakikisha wanaweka vyumba vya dharura kwa ajili ya washukiwa wa ugonjwa huo
Aidha, Nsanya amewataka wataalamu hao kutoa huduma kwa weledi na kusimamia mikakati iliyowekwa juu ya udhibiti wa ugonjwa wa ebola.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa