Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Peter Nsanya awapa siku tano wakuu wa vituo vya kutolea huduma za afya vilivyobainika kuwa na upotevu wa dawa kutoa maelezo ya waliohusika ikiambatana na mikakati ya kurejesha fedha hizo mara moja
Mganga Mkuu ametoa Kauli hiyo leo tarehe 5 Mei, 2021 kwenye kikao kazi kilichohusisha waganga wafawidhi wa vituo, wafamasia, wataalamu wa maabara na wauguzi kutoka vituo 20 vilivyofanywa ukaguzi wa dawa na vitendanishi na kukutwa na upotevu wa bidhaa hizo
Nsanya amesema kumekuwa na kawaida ya wahudumu wa afya kutofuata utaratibu wa uwekaji wa taarifa sahihi wakati utoaji wa bidhaa za dawa na vitendanishi kwa wateja hali inayopelekea kukosa mtiririko mzuri wa taarifa za bidhaa zilizopokelewa na zilizotumika.
Wataalamu wa afya kutoka vituoni.
"Nawapa siku tano Hadi kufikia tarehe 10 mwezi huu kila Mkuu wa kituo awe ameleta taarifa ya alivyochukua hatua Kwa waliosababisha upotevu huo poja na mikakati ya kurejesha fedha hizo atakayyeshindwa kufanya hivyo atachukuliwa hatua yeye kwa kushindwa kuwajibika kama kiongozi mkuu wa kituo " aliagiza Nsanya.
Akisoma taarifa ya ukaguzi maalumu wa bidhaa za afya Kwa kipindi cha mwezi julai hadi disema 2020, mfamasia wa Manispaa hiyo Magreth Mlai alisema katika ukaguzi upotevu wa dawa ulikuwa eneo la stoo , dawa zilizochina na bidhaa zilizozidi ambapo kwa eneo la stoo pekee kulikuwa na upotevu wa bidhaa za afya zenye zaidi ya thamani ya shilingi milioni 66 huku dawa zilizochina au kuisha muda wa matumizi kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10
Mfamasia wa Manispaa ya ubungo akiwasilisha taarifa ya ukaguzi
Mlai alisema baada ya ukaguzi timu iligundua kuwa sababu kubwa iliyopelekea kuwepo Kwa upotevu mkubwa wa bidhaa hizo ni kutotumia vizuri mfumo wa GotHomis pamoja kutotumia ipasavyo nyenzo za kutunzia kumbukumbu za matumizi ya bidhaa hizo.
"Tumieni nyenzo za utunzaji taarifa za bidhaa kuanzia stoo hadi hatua ya kumpa mteja hakikisha unaandika ili kuwa na taarifa sahihi za matumizi ya bidhaa hizo kwenye kituo" alisisitiza Mlai
Wakiongea Kwa nyakati tofauti wataalamu hao kutoka kwenye vituo vya kutolea huduma za afya wameahidi kutekeleza agizo hilo ikiwa ni pamoja na kuzingatia utaratibu wa utoaji dawa na vitendanishi ili kuondoa tatizo la upotevu ambalo limejitokeza katika kipindi hiki.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa