Leo tarehe 14 desemba, 2020 Manispaa ya Ubungo imewahamisha wajasiriamali wadogo zaidi ya 700 wanaofanya biashara zao barabarani eneo la mbezi kwenye mabanda ya wajasiriamali yaliyojengwa na Manispaa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali la kutenga maeneo maalumu ya wajasiriamali yatakayowawezesha kufanya Biashara zao kwa usalama.
Akiongea na wajasiriamali hao , Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic amesema kuwa zoezi limeanza leo rasmi kwa kuwagawia vizimba wajasiriamali ili kesho tarehe 15 desemba,2020 waanze kufanyia biashara zao hapo.
Wajasiriamali wakisikiliza kwa makini utaratibu wa kugawa vizimba kwenye soko la Mbezi Louis
"Baada ya kugawa vizimba hivi hatutegemei kumwona mfanyabiashara yeyote akifanya Biashara zake kandokando ya barabara na maeneo yasiyo rasmi katika eneo hili la Mbezi.
Beatrice ameendelea kueleza kuwa "baad ya zoezi hili kukamilika tunategemea wajasiriamali wote wataondoka barabarani kama Mheshimiwa Rais alivyosema watengewe maeneo maalum kama haya na sisi kama Manispaa tutalisimamia hili" nawasii wafanyabiashara wasijaribu kufanya biashara nje ya eneo hili maalumu kwani hatua zitachuliwa dhidi yake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic (wa kwanza kulia) akimuonesha kizimba moja ya wajasiriamali kwenye soko la mbezi
Beatrice ameainisha kuwa, wafanyabiashara watakao anza kuhamishwa ni wenye Biashara za matunda, mbogamboga na vyakula kwa ujumla huku wengine wakisubiri kidogo.
Aidha, Kila mfanyabiashara atawajibika kulipa shilingi 500 kila siku ikiwa ni gharama za usafi wa soko ukizingatia soko litahusisha uuzaji wa bidhaa za vyakula
Pia Beatrice kaeleza kuwa Ujenzi wa soko hili la wajasiriamali wadogo ni utekelezaji agizo la Mheshimiwa Rais ya kutengewa maeneo maalum ya kufanyia biashara zao ambapo Manispaa imetumia zaidi ya bilioni 900 kwa ajili ya kulipa fidia na kujenga mabanda hayo kwa zaidi shilingi milioni 600, fedha zote ikiwa ni mapato ya ndani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ubungo akiwafunda wajasiriamali wa Mbezi Louis kabla ya zoezi la kutoa maeneo ya kufanyia biashara.
Mtambue kuwa moja ya kazi ya kodi zinalipwa na wananchi wakiwemo wafanyabiashara ni kuboresha huduma Kwa wananchi " ndio maana Manispaa imeweza kujenga soko hili ambalo litawasaidia wajasiriamali kufanya biashara kwa utulivu"
Kwa upande wake Afisa Biashara wa Manispaa hiyo Prisca Mjema aliwaeleza wajasiriamali hao kuwa utambuzi wa wajasiriamali umefanywa na watendaji wa mtaa hivyo haki imetendeka hatutegemei kupata malalamiko.
Afisa biashara wa Manispaa ya Ubungo akifanya zoezi la kuhakiki wajasiriamali kabla ya kupewa eneo la kufanyia biashara.
Aidha Mjema amewasisitiza wajasiriamali hao kutambua kuwa uhamisho huo utawaondolea kibali cha kufanya biashara maeneo ya barabarani ili kupisha matumizi bora na salama ya barabara.
Akizungumza Kwa niaba ya wajasiliamali wenzake zuhura yusuph ameishukuru Manispaa Kwa kujenga mabanda hayo ambayo yatawasaidia kufanya biashara Kwa utulivu
"Jua na mvua vilikuwa halali yetu, lakini Kwa sasa tutaondokana navyo tutafanya biashara wakati wote bila mateso , asante Kwa Serikali ya awamu ya tano Kwa kutukimbukka wajasiriamali" alisema Zuhura.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa