Wamama wajawazito wametakiwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu ikiwemo ulaji wa lishe bora ili kupunguza tatizo la watoto kuzaliwa na uzito mdogo yaani chini ya kilo mbili na nusu hali ambayo ni hatari kwa maisha ya Mtoto
Rai hiyo imetolewa na wajumbe wa Kamati ya lishe ya Manispaa ya Ubungo baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2020/21 ilionesha kuwa asilimia 34.9 ya watoto waliozaliwa kwa kipindi hicho walikuwa na uzito chini ya kilo 2.5
Akizungumza wakati wa kikao hicho , Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James alisema ni vizuri akina mama wajawazito wakazingatia maelekezo ya wataalamu wa afya kuhusu afya ya mama na mtoto yanayotolewa kwenye vituo vyetu vya kutolea huduma za afya.
Aidha, Kheri amewataka wataalamu kuendelea kutoa Elimu ya lishe Kwa jamii kwani lishe duni ikimwathiri Mtoto Taifa limeathirika pia katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo kuwa na watu wasio na uelewa wa kutosha, kutumia fedha nyingi kwenye bajeti ya Afya. Ili kuhakikisha elimu ya lishe inawafikia makundi yote Kheri, amesisitiza uundwaji wa clabu za lishe kwenye shule zote za Msingi na Sekondari zitakozowasaidia kutambua umuhimu wa lishe wakiwa na umri mdogo kwani hilo ni Kati ya kundi linaloathirika zaidi na lishe duni.
Ameendelea Kwa kusema kuwa , Kamati na bodi za shule zipewe elimu ya lishe ili kuhamasisha wanafunzi kupata chakula shule pamoja na uanzishwa wa bustani za mbogamboga na matunda shuleni ili wanafunzi wanaokosa lishe nyumbani wapate shule lakini pia kujenga utamaduni wa kula vyakula vyenye lishe.
"Suala la lishe ni mtambuka ni lazima tushirikiane kwa pamoja katika kuhamasisha jamii kuzingatia lishe bora kuanzia ngazi ya jamii, viongozi wa dini na wataalamu katika kuhakikisha tunaepuka madhara yanayotoka na ulaji wa lishe duni ikiwemo, magonjwa ya ajili, watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa na migongo wazi pamoja na kuwa na watoto wenye uwezo mdogo kiakili.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa