Wajumbe wa baraza la Madiwani la Manispaa ya Ubungo wamewapongeza Mstahiki Meya na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kwa kununua Vishikwambi (tablets) Kwa ajili ya kutumia katika uendeshaji wa vikao na mikutano mbalimbali vya kisheria badala ya makablasha ya nakala ngumu.
Ununuzi wa vifaa hivyo umerahisha utumaji, utumiaji na utunzaji wa taarifa mbalimbali za vikao hivyo ukilinganisha na makablasha ya nakala ngumu ambayo ni rahisi kupotea, ugumu wa kutunza lakini pia gharama kubwa ya kuandaa na kusambaza.
Diwani wa Kata ya Mburahati Mheshimiwa Yusuph Omary Yenga alitoa pongezi hizo ambazo ziliungwa mkono na wajumbe wa Baraza hilo kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za Maendeleo ngazi ya kata katika kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2021/2022 uliofanyika leo Oktoba 28,2021
Mheshimiwa Yenga amesema kuwa matumizi ya vifaa hivyo yamerahisisha uendeshaji wa vikao kwani wajumbe wanapata nakala tete (soft copy) ya taarifa za na kufanya mijadala kupitia vifaa hivyo kwa haraka ukilinganisha upataji wa taarifa kwa njia ya makablasha ya nakala ngumu.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa