Mafunzo hayo yametolewa tarehe 6 mei 2021 katika ukumbi mikutano wa Manispaa ya Ubungo uliopo luguruni yakiwa na lengo la kuwaelimisha wajumbe namna ya kuendesha mabaraza katika kata zao wakizingatia sheria na kanuni ambazo zitasaidia katika uendeshaji wa mashauri na utoaji wa hukumu
Wakati wa mafunzo hayo Mwezeshaji Demetria Kabera ambaye pia ni mwanasheria wa Manispaa ya ubungo aliwasomea wajumbe muundo ambao unastahili kutumika na akidi ya wajumbe kutimia kwa kuzingatia sheria namba 7 ya mwaka 1985 sura ya 206 inayotaka wajumbe wa baraza hilo wasipungue wa 4 na wasiozidi 8 ili kutekeleza shughuli za baraza kwa ufanisi
Aliendelea kwa kusema kuwa dhumuni la mabaraza hayo katika kila kata ni kuleta amani na usuluhisho wa matatizo kwa wanachi ambao mnawahudumia.
Nae mwezeshaji kutoka ofisi ya mwekahazina wa Manispaa ya ubungo Esau Hosiana aliwapiga msasa wajumbe katika swala zima la tozo za ukusanya wa mapato ambazo mabaraza ya kata yanahusika ilikukusanya mapato ya serikali
Aliendelea kwa kusema kuwa "ni vyema tozo ambazo zinatakiwa kukusanywa zijulikane na tozo hizo lazima ziwe katka muhtasari ambao utawaongoza wajumbe" alisisitiza MwekahazinaSambamba na hayo hakimu mfawidhi wa mahakama ya mwanzo kimara Ndg. Furutuni Hamisi Aliwataka wajumbe kufuata taratibu na kuzingatia mashauri yenye haki kwa wananchi wao wanapotatua migogoro na bila kupendelea kwa kutoa haki kwa kila mtu
NB.mafunzo hayo yatafanyika siku mbili, leo jimbo la ubungo na kesho wajumbe wa jimbo la kibamba
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa