Waliopata kazi ya muda ya kukusanya taarifa za Anwani za makazi wametakiwa kwenda kufanya kazi hiyo kwa weledi , ufanisi na haraka katika zoezi hilo adhimu la Kitaifa.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James wakati akifungua mafunzo hayo leo tarehe 26/02/2022 katika ofisi ya Mkurugenzi na kuwasisitiza kuwa nafasi waliyooipata waitumie vizuri kwani wengi walitamani kupata nafasi hiyo.
Aidha James amewataka waandikishaji hao kuzingatia maadili ya katika utekelezaji wa kazi hiyo wakiwemo Viongozi na wananchi pindi watakapotembelea nyumba za Wananchi sambamba na Kupokea maelekezo ya Viongozi
Wamekumbushwa kutumia lugha nzuri wakati wa kuongea na Wananchi katika kuwaelewesha juu ya dhamira, malengo na namna ya kufanikisha zoezi hili muhimu nchini.
“Ni haki ya mwanachi kukudadisa ili aweze kupata taarifa za kumlidhisha na kukupa ushirikiano hivyo nendeni kwa nidhamu.” Alisema Mhe. James.
Nae Monica Medard Msugwa kwa niaba ya waandikishaji wengine amesema wamepokea maelekezo yote waliyopewa na Mkuu wa Wilaya na kuahidi kwenda kufanya kazi hiyo kwa weledi, ufanisi na haraka.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa