Wamiliki wa vituo vya watoto walio chini ya miaka mitano (DAYCARE) katika Manispaa ya Ubungo jijini Dar Es salaam, wamepatiwa mafunzo maalumu yanayolenga kufahamu sheria, kanuni na taratibu na miongozo ya uendeshaji wa vituo hivyo ili kutoa huduma bora ya malezi kwa watoto.
Mafunzo hayo yametolewa leo januari 23, 2021 na Manispaa ya Ubungo kupitia idara ya afya na ustawi wa jamii ambapo wamiliki 321 kati ya 600 wameshiriki mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Lapaz mtaa wa Luguluni.
Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana maarufu kama Daycare wapatiwa mafunzo juu ya taratibu kanuni na sheria za kuendesha vituo hivyo.
Akitoa maelezo wakati wa kufungua mafunzo hayo Afisa ustawi wa Manispaa ya Ubungo Zainabu Masilamba , alisema kuwa Manispaa kupitia kitengo cha ustawi wa jamii imeamua kuendesha mafunzo kwa wamiliki hao kutokana na ongezeko kubwa la uanzishwaji wa vituo hivyo vya kulelea watoto wadogo ambavyo havina usajili jambo ambalo ni kinyume na taratibu.
Masilamba alieleza kuwa, kwa mujibu wa kanuni za mwaka 2014 sura ya 13 kupitia sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 inaelekeza ili kituo cha kulelea watoto wadogo mchana kiweze kufanya kazi lazima kuzingatia vigezo ambavyo vitamwezesha mtoto kuwa katika mazingira salama ya kujifunza elimu ya malezi ya awali
Baada ya mafunzo haya ya kujenga uelewa, tunategemea wamiliki wa vituo ambavyo vinaendeshwa kinyume na taratibu, sheria na miongozo watatumia muda huu uliobaki kurekebisha kasoro zilizopo ili wasifungiwe vituo wakati wa zoezi la kufunga vituo visivyo na sifa mwishoni mwa mwezi machi.
Masilamba anasema " tarehe 24 machi mwaka huu, Manispaa ya Ubungo itafunga vituo vyote ambavyo vinaendesha huduma ya kulea watoto wadogo mchana kinyume na taratibu, kanuni miongozo na sheria ya kuendesha vituo hivyo ikwemo kutosajiliwa na kuto kidhi vigezo vya kutoa huduma ya malezi ya awali kwa watoto wadogo"
Aidha wamiliki wamekumbushwa kuzingatia ukubwa wa eneo litakalo mwezesha mtoto kujifunza kwa vitendo, uwepo wa miundombinu mizuri hasa vyoo, usafi wa mazingira na pamoja na kuwa na walezi waliopata mafunzo katika vyuo vya Montesol vinavyotambulika na serikali na kamishina wa ustawi wa jamii.
Wito umetolewa kwa wamiliki wa vituo vya kutoa huduma ya malezi ya awali kwa watoto wadogo mchana kutochanganya (daycare) na huduma zitolewazo katika shule za awali (nursery school) ikiwemo kuandika
Frank Andrea Kimaro ni kati ya wamiliki wa vituo waliopata mafunzo hayo, ameeleza kuwa mafunzo hayo yamemuongezea uelewa zaidi wa namna ya kuendesha kituo chake lakini pia vitu au huduma anayostahili mtoto mdogo kutoka kwenye kituo.
Manispaa ya Ubungo ina jumla ya vituo 606 vinavyotoa huduma ya kulea watoto wadogo mchana na kati hivyo ni vituo 100 vimesajiliwa
Mganga mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt Peter Nsanya akisisitiza jambo kwa wamiliki wa vituo wakati wa mafunzo. Amewakumbusha umuhimu wa kujiunga na bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa (iCHF) ili kuwa na uhakika wa matibabu kwa gharama nafuu.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa