Kutokana na kuwepo kwa mtindo usiofaa wa ulaji katika jamii, Wamiliki na wasimamizi wa vituo vya watoto walio chini ya miaka mitano (DAYCARE) katika Manispaa ya Ubungo jijini Dar Es salaam, wamepatiwa mafunzo ya umuhimu wa kuwapa lishe bora watoto wanapokuwa katika vituo pamoja na kuwafundisha ili wakue wakitambua umuhumu wa kula lishe bora tangu wakiwa wadogo.
Mafunzo hayo yametolewa leo Oktoba 23, 2022 na Afisa lishe wa Manispaa ya Ubungo ndugu Beatrice Mossile lengo ikiwa ni kuhakikisha wamiliki hao wanatambua mlo unaofaa kwa watoto wawapo vituoni hapo kwani ni hitaji la msingi kwa mtoto ili akue vizuri kiafya, kimwili na kiakili na hivyo kuondoa udumavu.
Mossile ameeleza kuwa, ulaji usiozingatia mlo kamili wenye makundi yote matano ya chakula yaani Protein, wanga, vitamin, madini na nishati ni chanzo kikubwa cha ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza sio kwa watu wazima tu bali hata watoto, hivyo lazima watoto wapate elimu ya lishe bora tangu wakiwa wadogo kutoka kwa walimu.
“Watoto wanamwamini sana mwalimu kuliko hata mzazi hivyo tunaamini wamiliki wa vituo vya kulelea watoto wadogo mkiwaelimisha lishe bora ni nini tutakuwa na jamii yenye afya njema, mfano watoto wengi hawapendi kula mboga za majani ambazo ni muhimu sana hivyo mtusaidie kuwaelekeza watoto” alisistiza Mossile
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa