Wamiliki wa baa na kumbi za burudani Manispaa ya Ubungo wametakiwa kufuata sheria na kanuni ya kukata vibali vya burudani vinavyowapa uhalali wa kufanya Biashara hiyo kwa kutumia kazi za Sanaa Kwa kuwa Sanaa ni kazi na ni Biashara Kama zilivyo Biashara zingine hivyo zinapaswa kulipa tozo.
Agizo Hilo limetolewa na Afisa utamaduni wa Manispaa hiyo,Ritha Nguruwe wakati wa ukaguzi wa maeneo ya burudani hizo na kuainisha kuwa Kumbi hizo ni pamoja na kumbi za sherehe, upigaji wa mziki wa vyombo(live band) hivyo wanatakiwa kulipa tozo za Vibali Kama sheria ndogo za Manispaa zinavyoelekeza
"Kwa sasa,tukiwa tunaelekea mwishoni mwa mwaka shughuli za burudani ni nyingi Sana hivyo tunawakumbusha na kuwaelekeza wamiliki wa kumbi za burudani na baa kuwa na vibali ili kulinda usalama wa mlaji wa kazi za Sanaa" ameeleza Nguruwe.
Nguruwe amesema kuwa, Wamiliki wengi wa sehemu za kutoa huduma za burudani hawafuati sheria ya kukata vibali ndio maana tumeamua kufanya ukaguzi wa kushtukiza ili kubaini wanaokwepa kulipa tozo Kwa wakati Kama Serikali inavyosisitiza ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali.
Aidha, Ritha amefafanua kuwa, Kumbi ambazo hazina zuio la sauti (sound proof) zinaruhisiwa kutoa burudani mpaka saa 6 usiku Kwa siku za jumamosi na jumapili huku siku za kawaida mwisho saa tano wakati zenye zuio la sauti zinaruhisiwa kutoa burudani zaidi ya masaa hayo.
Zoezi hili linatekelezwa na Manispaa Kwa mujibu wa sheria ndogo za Vibali vya burudani ambazo zinawataka wamiliki wa maeneo yanayotoa burudani kulipia Vibali vya kutoa burudani hizo ikiwa ni sehemu ya kuchangia mapato ya Manispaa na Kwa kutambua kazi za Sanaa.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa