Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori amewaagiza wamiliki wote wa mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani kuzifunga haraka Ofisi bubu wanazotumia kukatisha tiketi na kupakia abiria badala yake watumie Ofisi zilizopo kituo cha mabasi cha Magufuli kama sheria inayoelekeza.
Makori ametoa agizo hilo leo Aprili mosi kwenye kikao Kati ya wamiliki wa makampuni ya mabasi na uongozi wa Wilaya na Manispaa ya Ubungo na kueleza kuwa makampuni 24 yana Ofisi nje ya kituo cha Mabasi jambo ambalo ni kinyume na sheria.
"Nawapa siku tatu kampuni zote za mabasi zenye Ofisi za kukatisha tiketi na kupakia abiria nje ya kituo cha Mabasi cha Magufuli wafunge Ofisi hizo haraka atakayekiuka agizo hili hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kutozwa faini ya shilingi milioni moja kwa basi moja" amesisitiza Makori.
Makori aliendelea kusisitiza kuwa kitendo cha kupakia abiria nje ya kituo cha mabasi cha Magufuli ni ukwepaji wa kulipa Kodi ya Serikali jambo ambalo ni kinyume na Sera ya nchi inayosisiyiza ulipaji Kodi.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic amewahakikishi wamiliki wa makampuni ya mabasi hao kuendelea kuweka mazingira mazuri ya kibiashara ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya kituo hicho.
Akichangia kwenye kikao hicho mmiliki wa mabasi ya kampuni ya shabiby Afiz Said amesema kitendo cha baadhi ya wamiliki kuwa na Ofisi nje ya kituo cha mabasi pamoja na kuwa kinasababisha Serikali kupoteza mapato lakini pia sio haki kwa wamiliki waliotii sheria ya kuwa na Ofisi kwenye kituo kwani wanalipa Kodi nyingi zaidi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa