Katibu Tawala mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam Rehema Seif Madenge atembelea Manispaa ya Ubungo nakuongea na watumishi, apongeza utendaji kazi wa watumishi wa Manispaa hiyo na kusisitiza ushirikiano, upendo na uhusiano mzuri katika kazi
Aidha amesisitiza katika ukamilishwaji wa miradi na usimamizi mzuri na pia Kila mmoja kutekeleza wajibu wake awapo katika kituo Chake Cha kazi
Aidha, Rehema ameahidi ushirikiano na Kila mwenye changamoto asisite kuniona na tutafanya kazi kwa pamoja aliongeza
"Tujifunze kulindana na pale unapoona mwenzio anafanya sivyo tusaidiane kuwekana sawa" alisisitiza Rehema
Aliendelea kwa kusema kuwa, niwaombe mkatekeleze majukumu yetu kwa uweledi na hasa kwa kufata Sheria, kanuni na taratibu
Mimi ni sehemu ya nyinyi , Nimekuja kuwasikiliza na kuongea na ninyi mnipe mawazo yenu ili tuanze kazi kwa pamoja
Nae Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo ndugu, Beatrice Dominic ameshukuru kwa ujio wa katibu Tawala huyo kwa kutembelea Manispaa ya ubungo, nakumkaribisha tena
Halikadhalika, Beatrice amewakaribisha watumishi wote kushiriki katika tamasha la sensa ya watu na Makazi ambalo litafanyika kesho tarehe 20 agosti, 2022 katika viwanja vya Barafu - Mburahati
Nae Lusayo mwendawila, kwa niaba ya watumishi Manispaa ya Ubungo ameshukuru kwa ujio wa katibu Tawala huyo kusalimia wanaubungo na kuahidi kutekeleza maagizo yote ambayo yametolewa.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa