Mapema leo timu ya wataalam wa Jiolojia kutoka Taasisi ya Madini Tanzania ( GST) imewasili katika Mtaa wa makoka kata ya makubuli kujionea hali halisi ya tope linalobubujika na kuleta madhara kwa wananchi wa eneo hilo.
Gabliel Mbogoni ambaye ni Mjiorojia mwandamizi baada ya kutembelea eneo hilo amelezea kuwa utobubujikaji wa tope hilo ni moja ya majanga ya asili ambayo hutokea kwenye matabaka ya miamba hasa yenye udongo ambayo ikitikikiswa na matetemeko ya upitaji wa magari hupelekea ardhi kuwa katika hali hiyo.
Kutokana na Hali hiyo , Mbogoni amewataka wananchi wa eneo hilo na watumiaji wa barabara hiyo kuendelee kuchukua tahadhari pamoja na kuwa njia hiyo itajazwa mawe.
Aidha, Mbogoni ameelezea kuwa moja ya athari zinazoweza kujitokeza katika eneo hilo ni pamoja na nyumba kuzama na watu kupoteza maisha
Nae mwananchi wa eneo hilo Chalse Mtweve ameelezea hali halisi ya mazingira ya eneo hilo linavyowapa changamoto wananchi wa eneo hilo ikiwemo kukosa amani na hata kuhofia watoto wadogo wanaopita na kucheza katika eneo kwani wanaweza kudumbukia.
Kwa upande wake Bi Scolastika Bushoka mkazi wa Makoka ameeleza kuwa changamoto kubwa ya eneo hilo kuzama kwa magari hivyo kuleta hofu kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa