Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Angelina Manila amewataka Wananchi kuacha kuvamia na kujenga nyumba kwenye mashamba au maeneo wasiomiliki kwani hali hiyo inakwamisha mazoezi ya urasimishaji katika maeneo mengi
Naibu waziri alitoa kauli hiyo Novemba 03,2021 kwenye Mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi uliofanyika Mtaa wa Kwa Yusuph kata ya Msigani Manispaa ya ubungo na kusema kuwa katika utaratibu wa urasimishaji ardhi eneo linalasimishwa mara moja ili lilasimishwe upya ni lazima hati ya awali ifutwe
"Kwa ubungo changamoto hii ipo na inachangia Kwa kiasi kikubwa ucheleweshwaji wa upangaji na upimaji wa maeneo hivyo ni lazima jambo hili lifanyike kazi Kwa wale walioko kwenye maeneo hayo ili kuyawezesha Makampuni kufanya kazi yake kwa wakati" alifafanua Mhe.Mabula
Aidha, Naibu Waziri amekabidhi hati 32 za umiliki wa ardhi kwa wananchi wa Mtaa wa Kwa Yusuph na Malambamawili katika kata ya Msigani ikiwa ni mwendelezo wa kuhakikisha wananchi wanamilikishwa maeneo yao kisheria.
Ili kuhakikisha Mpango wa urasimishaji unakamilika ifikapo 2023, Serikali imefikia uamuzi wa kushirikiana na mabenki Kwa kuwakopesha fedha wananchi Kwa ajili ya kugharamia urasimisha wa maeneo yao kutokana na wananchi wengi kutomudu gharama hizo ambapo Kwa sasa zoezi hilo linatekelezwa Wilaya ya mbalali Mkoani Mbeya.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa