- Mapema leo Novemba 21, 2022 Manispaa ya Ubungo imeendesha zoezi la kubomoa ujenzi wa Kanisa la God's Family linalomilikiwa na ndugu Charles Mwaihojo lililopo Eneo la Kinzudi kata ya Goba
- Zoezi hilo limefanyika kufuatia Manispaa kushinda kesi iliyokuwa imefunguliwa katika mahakama kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi Na ndugu Charles Mwaihojo ambapo alikua akilalamika kutoruhusiwa kujenga kanisa katika eneo hilo
- Awali eneo hilo lilitolewa kibali cha ujenzi kwaajili ya makazi badala yake mmiliki aligeuza matumizi ya eneo hilo na kuanza kujenga kanisa jambo ambalo lilikua linaenda kinyume na maombi ya kibali cha ujenzi kilichotolewa kwa eneo hilo. Zaidi ya hapo eneo hilo ni la makazi tu na haliruhusiwi kufanya ujenzi wa huduma za jamii
- Mmiliki wa Kanisa hilo alipeleka shauri mahakamani lakini alishindwa kesi hiyo hivyo basi Manispaa ya Ubungo imechukua hatua hiyo ya kubomoa baada ya mmiliki kushindwa kufanya hivo kwa muda aliopewa pamoja na kuonywa mara nyingi kwa maandishi na vikao pia
- Aidha kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo juu ya kelele zinazosababishwa na vyombo pamoja na spika zilizokuwa zimefungwa katika kanisa hilo ambalo lipo jirani kabisa na wananchi
- Manispaa ya Ubungo inaendelea kutoa rai kwa wananchi wake kuhakikisha wanapata vibali vya ujenzi kabla ya kuanza ujenzi wao, lakini pia wahakikishe wanafanya ujenzi wao kulingana na utaratibu wa vibali vyao ili kuepusha usumbufu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa