Zoezi la usafi wa mwisho wa Mwezi kwa Wilaya ya Ubungo limefanyika mapema leo katika Kata ya Goba na Wananchi wa Goba wameshiriki kwa wingi katika zoezi na kupongezwa kwa ushiriki wao
Aidha, katika zoezi Hilo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James ameendelea kuwasititiza mwananchi yoyote ambae hajahesabiwa ni lazima atafikiwa kwa sababu yoyote ile kwani hata siku za kuhesabu watu zikiisha na kuna mwananchi hajahesabiwa lazima afatwe kuhesabiwa kwa siku zijazo
Aliendelea kwa kusema kuwa, taarifa hizo zitasaidia serikali kupanga maendeleo na kuboresha ufanisi wa huduma katika wilaya hiyo.
Kheri, amewaeleza wananchi kua zoezi la sensa hadi sasa kulingana na taarifa kutoka serikalini ni kwamba zoezi linaenda vizuri sana katika wilaya ya ubungo huku akiwasisitizia viongozi wote wa serikali za mtaa na wananchi kutoa msaada kwa makarani ili kuwafikia wananchi wote na kusaidia zoezi hilo liende kwa haraka na ufanisi mzuri.
"Hakuna mwananchi ambae hatahesabiwa, wote mtahesabiwa kikubwa ni kutoa ushirikiano kwa makarani na viongozi wa serikali za mtaa ili kuhakikisha zoezi hili linaenda kwa haraka na kwa ufanisi tunaotarajia. "
Kheri, amewapongeza na kuwashukuru wananchi wote waliojitokeza kushiriki zoezi la usafi katika kata ya Goba asubuhi ya leo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa