Wakati maadhimisho ya siku ya wanawake yakiendelea katika maeneo mbalimbali nchini, wanawake wa Kata ya Saranga Manispaa ya Ubungo kupitia kikundi cha kituo cha Taarifa na Maarifa wamejipanga kuanzisha kiwanda cha kuchakata taka Kwa ajili ya kujiongezea kipato na kutunza mazingira.
Akieleza kwenye Maadhimisho hayo mmoja wa wanakikundi hicho alisema waliamua kuanzisha mradi huo baada ya kuona Uwepo wa taka nyingi ambazo zinaweza kugeuzwa mbolea asili na kufanya mazingira kuwa Safi na kuwezesha kikundi hicho kufikia malengo,
Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Dkt. Peter Nsanya alishiriki maadhimisho hayo na kuwapongeza Kwa wazo zuri la kuanzisha kiwanda cha kuchakata taka na kuwataka kuchangamkia fursa ya kupata mikopo isiyo na riba inayotolewa na Manispaa ili kukuza mtaji wa kiwanda Chao na hatimaye kufikia malengo.
Dkt.Nsanya aliendelea kuwambusha Watendaji wa Kata na Mitaa kusimamia vizuri swala la ullinzi na Usalama katika maeneo yao ili kuepusha vitendo vya ubakaji vinavyotokea kwenye mitaa hasa nyakaji za usiku
"Imarisheni ULINZI shirikishi ili kukomesha vitendo hivi ambavyo vinawaathiri Sana wakinamama na watoto" alielekeza Dkt. Nsanya
Dkt Nsanya ametumia pia fursa hiyo kuwakumbusha Watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha Machinga hawarudi kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi kufanya biashara ili kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kutaja Machinga wawe kwenye maeneo rasmi ya kufanya biashara.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa