Vikundi vya Vijana na Watu Wenye Ulemavu Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo vinavyotarajia kupewa mkopo usio na riba kufanya marekesho kwa wakati ili kutoa fursa kwa wananchi wengine kunufaika na mfuko huo unaotokana na asilimia kumi [10%] ya mapato ya ndanj ya Halmashauri hiyo.
Rai hiyo ameitoa Afisa Maendeleo wa Manispaa ya hiyo Rose Mpeleta kwenye kikao kilichohusisha vikundi vinavvyotarajia kupata mkopo wa vyombo vya moto yaani bodaboda na bajaji na kueleza kuwa watapaswa kuanza kufanya marekesho wiki mbili baada ya kukabidhiwa vyombo hivyo.
Halmashauri inatarajia kutoa bajaji 13 na bodaboda 16 zenye thamani ya shilingi Millioni 123 lengo ikiwa ni kuviwezesha vikundi hivyo kujikwamua kiuchimi kupitia vyombo hivyo.
"Tambueni kuwa fedha zitakazotumika kununua vyombo hivyo ni Mali ya Serikali na lengo ni kuwakwamu kiuchumi sio sadaka mnapaswa kurejesha kwa wakati kwa mujibu wa makubaliano ili na wengine wakopeshwe" alisema Mpereta
Aidha Mpeleta amesema, Kwa sasa Wanufaika wote watakao pata mikopo ya vyombo vya Moto wanatakiwa kufanya marejesho ya mikopo yao kila baada ya wiki mbili mara baada ya kuka bidhiwa vyombo hivyo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa