Ili kujenga dhana ya umiliki wa miradi ya maendeleo kwa wananchi, viongozi na wataalamu wa maeneo yenye miradi Wana wajibu wa kuhakikisha wananchi wanashirikishwa ipasavyo kuanzia hatua za awali hadi kukamilika kwake.
Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Ubungo mhe. Kheri James baada ya kufanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata ya Kimara ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake aliyoianza Jana agosti 25,2021
"Mwananchi akishirikishwa kwenye miradi inayotekelezwa kwenye eneo lake inajenga uelewa lakini pia kupunguza malalamiko yanayosababisha wananchi kuto ipenda serikali yao, itisheni mikutano ili kuwapa taarifa za maendeleo wananchi katika mitaa yenu" alieleza kheri.
Ipo miradi inayotekelezwa kwa nguvu za wananchi baada ya kushirikishwa juu ya uhitaji wa huduma kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo mradi wa ujenzi wa kituo Cha polisi mtaa wa mavulunza kwa nguvu za wananchi, "tuwashirikishe kwa umoja wetu tutafanya mengi" alieleza kheri
Kheri ameendelea kuwakumbusha viongozi na wataalamu hao kuhakikisha wanashughilikia vizuri na kwa wakati kero za wananchi ili kujenga imani kwa wananchi juu ya serikali yao.
Aidha, Mkuu wa Wilaya amewakumbusha viongozi hao kuwajibika katika majukumu yao ikiwemo ukusanyaji wa mapato, kusimamia ulinzi na usalama, usafi wa mazingira pamoja na usimamizi wa miradi ya ya maendeleo kwani ndio majukumu makuu katika kuwahudumia wananchi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa