Maafisa Kilimo Manispaa ya Ubungo Leo tarehe 23.11.2021 wamepewa Elimu kuhusu maswala ya lishe na usindikaji wa vyakula mbalimbali ili kuwawezesha kuwa na uelewa mzuri wa kutoa elimu kwa wananchi
Akitoa mafunzo hayo Afisa Kilimo katika maswala ya lishe Bi.Stela Nzelu ameeleza kuwa wataalam wa Kilimo wanawajibu kuelimisha wakulima na wasindikaji kuzingatia lishe kwenye vyakula
Ili kuwa na Jamii au Taifa lenye maendeleo ni muhimu Jamii kula vyakula vinavyozingatia makundi ya lishe Bora ili kuipa miili Kinga na Tiba dhidi ya magonjwa mbalimbali.Alieleza Stela
Aliendelea kufafanua rangi za Mazao na faida Stela alisema vyakula vyenye rangi ya Njano- vina wingi wa vitamini A, C na viondoa sumu, Rangi ya kijani- Kama Kinga Tiba kwa inni( njegere, mbogamboga tango bamia,kabegi,)
Vyenye Rangi nyeupe- kama Kinga na Tiba kwa mapafu( vitamini C' K, viondoa sumu ) mahindi vitungu,stafeli, Rangi nyeusi- Kinga na Tiba ya Figo,( bilinganya zambarau n.k na vyenye rangi nyekundu- Kama Kinga na Tiba ya moyo kitunguu, pilipili,nyanya, tikiti, bitroot,
Pia alitoa msisitizo wa ulaji wa mboga za majani uanzie utotoni ili kuwajengea Kinga nzuri ya mwili ili kuepukana na magonjwa hatarishi Kama moyo,ini n.k
Aidha Afisa Kilimo,umwagiliaji na Ushirika Manispaa ya Ubungo Happiness Mbelle aliwasisitiza wataalam hao kuendelea kuelimisha umma kuhusu uhifadhi wa vyakula na kuongeza uzalishaji wa mazao zaidi kwaajili ya kukabiliana na mabadiliko ya Hali ya hewa
Aliendelea kuwakumbusha Kutumia vyakula vyenye lishe Bora kwa Msingi wa kuongeza uzalishaji zaidi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa