- Leo Desemba 15, 2022 wataalamu wa afya kutokea ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wamefanya ziara ya ukaguzi wa vituo vya afya 6 vya Manispaa ya Ubungo
- Ziara hiyo ilikua ni mahsusi kwaajili ya kukagua utekelezaji wa mbinu mpya ya kuimarisha ubora wa takwimu za dawa ili ubora utumike kwenye kupanga na kutatua changamoto za upatikanaji wa dawa kwenye zahanati na vituo vya afya.
- Mnamo mwezi Septemba 2022 TAMISEMI kwa kushirikiana na shirika la UNFPA walitoa mafunzo kwa wataalamu wa afya kutoka vituo 16 vya Manispaa ya Ubungo kuhusu mpango huu muhimu kwaajili ya kutunza takwimu za dawa na uwezo wa kufanya maamuzi ili dawa zitumike ipasavyo kwenye Zahanati na vituo vya afya. Hivyo basi timu hii ya TAMISEMI imefanya ukaguzi huo ili kujiridhisha na utekelezaji wa mpango huo
- Akiongea katika ziara hiyo
Mkuu wa kitengo cha dawa na huduma za afya za kiuchunguzi TAMISEMI ndugu Mathew Mganga amesema kuwa mpango ni muhimu sana kutekelezwa ipasavyo katika zahanati, hospitali na vituo vyote vya afya ili kuhakikisha wanadhibiti tatizo la kuisha muda kwa dawa pamoja na kutunza mapato. Pia Ndugu Mganga amesema mpango huu utasaidia kurahisisha upatikanaji wa dawa husika kati ya kituo na kituo.- Kwa vituo vyote walivyotembelea kwa Manispaa ya Ubungo, timu hiyo imeridhishwa na utekelezaji wa mpango kwa Manispaa ya Ubungo na wamewapongeza wataalamu wote wa Afya na Manispaa kwa ujumla
@ortamisemi
@wizara_afyatz
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa