- Mapema leo Novemba 24, 2022 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James amefanya kikao kazi na watendaji wa kata zote 14 za Manispaa ya Ubungo kuhusu ajenda kuu ya usafi wa mazingira katika mitaa yote
- Katika kikao hicho James amewakumbusha watendaji hao juu ya nafasi kubwa walonayo ya kuwasimamia watendaji wa mitaa ili kuitekeleza kwa nguvu ajenda ya usafi wa mazingira ambayo bado kuna changamoto kwenye utekelezaji wake
- Akiongea katika kikao hicho James amesema kuwa bado kuna changamoto kadhaa kwenye baadhi ya mitaa yetu, changamoto ikiwemo utiririshaji wa maji machafu kwenye barabara, uuzaji wa biashara ndogondogo kiholela, bajaji kupaki kiholela pamoja na wafanyabiashara kurudi kwenye maeneo yaliyokatazwa kufanya biashara.
"Bado maeneo kama Mbezi na Manzese kuna changamoto kubwa ya wafanyabiashara kurudi kwenye maeneo waliyokatazwa hivyo basi Watendaji lazima muhakikishe maeneo hayo yanarudi kuwa masafi na kuwapeleka wafanyabiashara kwenye maeneo waliyopangwa" alisema
- Naye afisa mazingira wa Manispaa ya Ubungo ndugu Lawi Benard amewataka watendaji hao wa kata kutorudi nyuma kwenye ajenda ya usafi na wahakikishe maeneo yao wanayosimamia yawe masafi kwa muda wote. Benard ameongeza kuwa Manispaa inajipanga kupanda miti pembezoni mwa barabara ya Morogoro ili kuleta mandhari mazuri ya wilaya ya Ubungo
- Akichangia katika kikao hicho Afisa biashara Manispaa ya Ubungo ndugu Merry Mwakyosi amewaomba watendaji hao kutoa ushirikiano mkubwa kwenye kutoa taarifa ya wafanyabiashara ambao hawana leseni katika maeneo yao hali inayopelekea kuikosesha Manispaa mapato
- Kampeni ya usafi wa mwisho wa mwezi kiwilaya inatarajiwa kufanyika Jumamosi ya Novemba 26 katika kata ya Mbezi eneo la njiapanda ya Goba hadi kituo cha Mabasi cha Magufuli ambapo mgeni rasmi atakua ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa