Manispaa ya Ubungo kupitia Idara ya Afya kitengo cha Lishe imewapa mikataba watendaji wa Kata za Manispaa hiyo lengo ikiwa ni kuendelea kusimamia mikakati ya Serikali juu ya suala la lishe bora kwa raia wake.
Usainishwaji huo umefanyika Leo tarehe 31 Oktoba, 2022 ambapo Watendaji Kata hao wamesaini mikataba hiyo yao na Manispaa hiyo na kutakiwa kwenda kuifanyia kazi kama mikataba hiyo inavyojieleza.
Akiongea Bi. Beatrice Mossile Afisa lishe wa Manispaa hiyo wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa lishe kwa ngazi ya Halmashauri kwa robo ya kwanza 2022/2023 amesema Kitengo cha lishe kimefanikiwa kutoa elimu kwa Madiwani 19, walimu wakuu wa Shule za msingi na Sekondari, walimu wa day care na walimu wa afya na kutibu utapiamlo.
Na hivyo kupelekea kuwepo kwa Shule 192 zenye club za afya na lishe Sawa na 74.4% kati ya Shule 258, Shule 90 za msingi na Sekondari zinazotumia unga wa mahindi uliowekwa virutubisho na kuwepo kwa mashine 7 za kusaga lishe sawa na 70% kati ya 10 zinazohitajika.
Mossile ameendelea kueleza kuwa Manispaa hiyo kwa sasa imefanikiwa kupambana na tatizo la udumavu kutoka 8% hadi kufikia 1.1% na hivyo matarajio ya Manispaa kwa sasa ni kuhakikisha idara ya elimu msingi na sekondari wanashirikiana vizuri na Kamati za shule, wazazi au walezi ili kukubaliana namna ya kuwezesha wanafunzi kupata chakula mashuleni kama muongozo wa lishe unavyoeleza.
Kwa upande wake Mhe. Kheri James Mkuu wa Wilaya ya Ubungo amesema ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha mpango wa lishe unasimamiwa vizuri na ametoa pongezi kwa Manispaa kwa kufanikiwa kupanbana na udumavu kutoka 8% hadi kufikia 1.1% na amezipongeza kata zilizofanya vizuri na ametoa wito kwa Kata zingine kuiga mfano wa Kata hizo.
James amewataka watendaji hao kuhakikisha wanafanya vikao na watendaji wa mitaa na walimu wakuu wa shule za kwenye maeneo yao, Kamati za shule, wazazi au walezi ili kujua namna bora ya kuwezesha watoto kupata chakula mashuleni.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa