Mkurugenzi Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic, amewataka watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha wanasimamia usafi katika maeneo yao kwani maeneo mengi ni machafu.
Agizo hilo amelitoa leo Julai 26,2021 kwenye kikao kazi kilichohusisha watendaji wa kata na Mitaa pamoja na Wenyeviti wa Mitaa wa Manispaa hiyo kilicholenga kuwakumbusha majukumu yao ikiwemo Usafi, Usimamizi wa miradi ya maendeleo, Ulinzi na usalama pamoja na masuala mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao
Amesema kuwa Kuna watendaji hawasimamii kabisa usafi katika maeneo yao hususani maeneo wazi *( smart area)* jambo ambalo ni kinyume na maagizo ya Mkuu wa Mkoa ya kuhakikisha Mitaa yote inakuwa misafi wakati wote.
"Watendaji acheni kukaa maofisini tokeni mkasimamie usafi katika Mitaa maeneo yenu kwani maeneo yenu mengi ni machafu na ni wajibu wenu kusimamia" Alisema Beatrice
Aidha Watendaji hao kuwakumbusha kuwa suala la usafi ni ajenda ya kudumu shirikisheni wananchi na wafanyabiashara kufanya usafi maeneo yao ili kufanya mazingira kuwa Safi kama maelekezo ya Mkoa yanavyosisitiza.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa