Watendaji wa kata na Mitaa Manispaa ya Ubungo jijini Dar Es salaam waagizwa kutambua na kuwasilisha halmashauri takwimu za majengo na mabango yaliyopo kwenye mitaa yao ifikapo tarehe 28 februari mwaka huu kwa ajili ya kuanza zoezi la kukusanya kodi.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori jana februari 9, 2021 kwenye kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa little flower eneo la mbezi kwa viongozi na watendaji hao kuanza zoezi hilo mapema iwezejanavyo ili Kodi hizo ziweze kukusanywa kama Serikali ilivyoelekeza.
Nimeona tukutane tupeane maelekezo na muda wa kutekeleza agizo hili kwa kuanza kutambua nyumba na mabango yaliyopo kwenye mitaa yenu kwa haraka na uaminifu mkubwa na atakayekwamisha atachukuliwa hatua" alieleza Kisare
Kisare amesema kuwa baada ya kupata takwimu hizo, Manispaa itaanza kampeni ya kukusanya Kodi hizo tarehe 22 Machi, 2021. “Tambueni kuwa serikali inajiendesha kupitia kodi kwa kiasi kikubwa hasa baada ya kuingia uchumi wa kati, hivyo ni lazima zoezi hili lifanyike kwa umakini za uaminifu mkubwa ili serikali ipate mapato”
Makori amewasisitiza watendaji hao kuwa zoezi hilo linahitaji umakini mkubwa Sana asionewe wala kupendelea mtu, “sitegemei kupata malalamiko kwa wananchi , zingatieni muongozo mtakaopewa na viongozi wenu"
Akiongea kwa niaba ya watendaji wengine , Mtendaji wa Kata ya Goba Musilima Mwenda alisema wamepokea agizo na watatekeleza kwa wakati hadi kufikia tarehe 28 mwezi huu takwimu zote zitakuwa zimekusanywa na kuwasilishwa kwa ajili ya kuanza zoezi la kukusanya kodi hizo tarehe 22 Machi kama ilivyoelekezwa.
Zoezi hili linalenga kuongeza wigo wa kukusanya mapato kutokana na uwanda wa serikali za mitaa kuwa mpana zaidi na kuyafikia majengo yaliyokusudiwa.
Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa ilitoa muongozo Mpya wa juu ya ukusanyaji wa Kodi za majengo na mabango kutekelezwa na Halmashauri nchini februari Mosi, 2021.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa