Baraza la madiwani Manispaa ya Ubungo la wapongeza watendaji wa kata zote 14 za Manispaa ya Ubungo kwa utendaji mzuri wa majukumu yao na ushirikiano mzuri kwa madiwani wa kata hizo na kuwaasa waendeleze juhudi hizo ili kuendelea kuleta maendeleo katika Manispaa hiyo
Pongezi hizo zimetolewa Leo 25 januari, 2022 wakati wa baraza la kupokea taarifa za Kata ambapo madiwani wa Kata zote huwasilisha taarifa hizo
Aidha Baraza hilo limependekeza watendaji waweze kununuliwa pikipiki ili kurahisisha ufanyaji wa kazi
Mbunge wa Kibamba Issa Mtemvu amepongeza Uongozi wa Manispaa ya Ubungo kwa kufanikiwa kuwawezesha madiwani kupata Vishikwambi ambavyo vinarahisisha upataji wa taarifa na pia kuweza kuendesha vikao kwa urahisi
Nae Mbunge wa Ubungo Kitila Mkumbo amesisitiza bajeti inayofanyiwa kazi sasa iweze kuwazingatia mahitaji ya watendaji ikiwemo Pikipiki kwani miundombinu yao ya ufanyaji kazi ni migumu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa