Kufuatia kifo cha aliyekuwa Mtendaji wa mtaaa wa Msumi kata ya Mbezi Kelvin Mowo aliyekufa baada ya kukatwa na mapanga na watu wasiojulikana akiwa ofisini kwake siku ya tareh 11oktoba 2021, watendaji wa kata na mitaa wa mkoa wa dar es salaam wamekubaliana kuanza kuadhimisha siku ya mtendaji kila tarehe 11 mwezi oktob ya kila mwaka kwa kutoa tuzo ya heshima kwa kwa kila mtendaji anayepitia changamoto katika kutekeleza majukumu yake wakianza na marehemu Kelvin Mowo
makubaliano hayo wameyafanya tarehe 14.10.2021 wakati wakitoa salamu za pole kwa familia na serikali kwa mtendaji mwenzao aliyepoteza maisha akiwa kazini akihudumia wananchi
Tumeamua kuanzisha tuzo hii ikiwa ni namna ya kumkumbuka ndugu na mtumishi mwenzetu Kelvin Mowo aliyepata umauti akiwa kazini kwa kushambuliwa tuzo hiyo itaitwa MOWO
Akiongea wakati salamu hizo mtendaji kutoka manispaa ya kinondoni Frank Kalinga alieleza kuwa jamii inapaswa kufahamu kuwa watendaji wa kata na mitaa ni wanajamii wenzao na sio maadui
shambulio hili sio la kelvin Mowo bali ni shambulio la watendaji wote tunaomba haki ikatendeke kwa wale waliohusika na kifo hiki kwa hatua za kisheria. alieleza Kalinga
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa