Watumishi hao waliosimamishwa kazi ni pamoja na Rose A. Mpeleta Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Allen Mjindo Afisa maendeleo ya jamii kata ya kwembe, Edger Msuya Afisa biashara, Amon Mboka Mhasibu wa Mikopo, Yusta Yongole Afisa maendeleo ya jamii kata ya mabibo, Evelyne Mangweha Afisa Maendeleo ya jamii na msajili wa vikundi, happiness Mwamakula afisa maendeleo ya jamii na mratibu wa mikopo ya vikundi na Juliana Kibonde afisa maendeleo ya jamii na msajili wa NGO’s.
Aidha, baraza limeazimia kuwa maafisa maendeleo ya jamii waliohamishwa vituo vya kazi warudi kwenye vituo vyao vya zamani ili wakasimamie marejesho ya mikopo ya vikundi kwa kipindi cha miezi mitatu na wakishindwa wachukuliwe hatua.
Baraza limewataka watumishi wote kutekeleza wajibu wao kwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni ya utumishi wa umma.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa