Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ubungo na Kibamba Beatrice Dominic amewataka Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika Uchaguzi mkuu ujao kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uadilifu na pamoja na kuzingatia miongozo na maelekezo yatakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili zoezi la uchaguzi liende vizuri.
Maelekezo hayo yametolewa leo wakati akifungua semina elekezi kwa wasimamizi hao wa vituo vya kupigia kura iliyofanyika Leo tarehe 23 oktoba ,2020 katika kumbi za chuo kikuu cha Dar es salama
Msimamizi msaidizi jimbo LA Ubungo Kissah Mbilla akitoa mafunzo elekezi kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura.
Beatrice amewaeleza Wasimamizi hao wa vituo vya kupigia kura kuwa, kushindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo kunaweza kusababisha vurugu, malalamiko au kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi, "hivyo ili Uchaguzi ufanyike Kwa amani na haki zingatieni Sheria, miongozo na taratibu za uchaguzi"
Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura wakisikiliza kwa makini maelekezo ya namna ya kusimamia uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 oktoba,2020
Aidha, Wasimamizi na Wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura wana wajibu wa kuhakikisha utulivu na usalama unakuwepo muda wote kwenye kituo cha kupigia kura, hii itafanya wapige kura kwa Uhuru na amani.
"Mkitumia madaraka yenu vizuri mtasaidia kuondoa migogoro inayoepukika na kufanya zoezi la uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kuwa la mafanikio makubwa" alieleza Beatrice
Aidha, Beatrice amewasisitiza Wasimamizi wa vituo hao kuheshimu viapo walivyo apa vya kutunza Siri na kujitoa uanachama wa vyama vya siasa wakati wote kuanzia, wakati wa mafunzo, Uchaguzi na baada ya zoezi la uchaguzi kumalizika.
Manispaa ya Ubungo ina jumla ya vituo 1545 vya kupigia kupigia kura Kwa Jimbo la Ubungo na Kibamba.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa