Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina tarehe 2/8/2020 atembelea banda la Ubungo kujionea kilimo cha kisasa, mashine za kisasa za kilimo na wajasiriamali wa kilimo, mifugo, uvuvi na usindikaji na kupokelewa na mwenyeji wake ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic, Afisa Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Happiness Mbelle na watumishi wa Manispaa hiyo.
Wakati akitembelea mabanda hayo Waziri aliipongeza Manispaa ya Ubungo kwa kuonyesha utofauti kwa kuweka banda la Afya ambalo linatoa huduma kwa wakulima na wafugaji bure na kwa mtu yeyote atakaye tembelea banda la Ubungo.
Aidha Waziri alimshauri Mkurugenzi atenge eneo kwa ajili ya wafugaji katika eneo linalomilikiwa na Halmashauri lililopo Kibesa.
Vilevile Waziri alisema kuwa baadhi ya vitu ambavyo vimekuwa vivutio ni mtambo unaotumia umeme wa upepo (windmill generator) mtambo huu unaweza kutoa maji kwa njia ya upepo na yakatumika kwa umwagiliaji.
Sambamba na hayo kilimo cha nyumba ya kijani (Green House) ambacho kina mazao kama nyanya, matango, letusi ya kijani, letusi nyekundu na col flower. Aliongeza Waziri
Wakati huohuo banda la ubungo limeendelea kupokea wageni tofauti tofauti ambao wanakuja kutembelea banda hilo
Mwisho Mhe. Waziri alikata keki na kula pamoja na watumishi na wajasiriamali.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa