• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Ubungo Municipal Council
Ubungo Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Malengo na dhamira
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Sekondari
      • Kilimo umwagiliaji na ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Mipango miji na Ardhi
      • Elimu Msingi
      • Utumishi na Utawala
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Maendeleo ya Jamii na Vijana
      • Maji na Usafishaji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Mazingira na udhibiti wa taka ngumu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA
        • Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Manunuzi na Ugavi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Masoko
    • Vituo vya Basi
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
      • Ushuru wa Huduma
      • Usajili wa Tax
      • Leseni za Biashara
      • Ushuru wa Hoteli
    • Ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
      • UJUWA
  • Madiwani
    • Orodha za Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba za vikao vya kisheria
    • Ratiba ya Kumuona Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi endelevu
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Ripoti
    • Sheria
    • Bronchures
    • Zabuni iliyotangazwa
    • Mpango Mkakati
    • Newsletter
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

WILAYA YA UBUNGO YAFANYA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA WILAYA KWA AJILI YA KUPITIA BAJETI NA KUISHAURI HALMASHAURI

Posted on: February 3rd, 2020

Leo hii Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya yaani DCC lengo kuu likiwa ni kupata maoni na ushauri kutoka kwa wajumbe kuhusu bajeti ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2020/2021.Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi uliopo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Mhe. Kisare aliambatana na Katibu Tawala Ndg. James Mkumbo na Mkurugenzi wa Manispaa  Beatrice Dominic na wajumbe wengine waliohudhuria ni viongozi wa vyama vya siasa, wakuu wa Idara na watendaji.

Wakati akifungua kikao hicho Mwenyekiti aliwasisitiza wajumbe kuwa lengo kuu la kikao ni kushauri katika maeneo ambayo pia wanaona yanastahili marekebisho na Wilaya itatilia mkazo na kuyafanyia kazi.

Aliongeza kuwa shughuli za vyama vya siasa zinafanywa kwa mujibu wa sheria na ndio maana viongozi wanakuwa wajumbe ili kusaidia kuleta maendeleo katika Wilaya.

''Hata Mhe. Rais amekuwa akisisitiza kuwa maendeleo hayana Chama, na ndio maana leo tuko wote hapa kwa ajili ya kumsaidia kuleta maendeleo ya Wilaya yetu” Aliongeza Mkuu wa Wilaya.

Aliwaambia pia kuwa nia nyingine ni kuhakikisha uongozi wa Halmashauri unatekeleza majukumu yake ipasavyo.

Katika kuchangia Mjumbe Coaster J. Kibonde ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia Makini Wilaya ya Ubungo alisema kuwa amefurahishwa kwa namna serikali ya awamu ya tano chini ya Mhe. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli inavyotekeleza miradi ya maendeleo na wananchi wanaiona. *”Nikuombe Mhe. Mkuu wa Wilaya kwa kuwa tunaamini kuwa wewe ni msikivu, wakati wa ziara za kutembelea miradi ya maendeleo na sisi kutoka vyama vingine vya siasa tualikwe ili tukawe mashuhuda wazuri wa namna mnavyotekeleza Ilani”* alisema Ndg. Coaster.

Mjumbe mwingine ambaye ni Katibu wa ACT wazalendo Ndg. Kassim Chogamawano aliiomba Halmashauri kutenga fedha ili kumalizia mradi wa machinjio Manzese pamoja na kuwa na fedha iliyotengwa kwa ajili ya machinjio ya kisasa Kibesa.

Mhe. Kisare aliwaomba wajumbe kufuata Utawala wa Sheria na kuwashukuru kwa kujitokeza kwao. Aliwasisitiza kutosubiri hadi kikao kitokee ili kujadili masuala mazima ya maendeleo kwani ofisi yake na Ofisi ya Mkurugenzi zipo wazi kwa ajili ya kusikiliza wananchi Kwa Maendeleo ya Ubungo.

Taarifa

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA DEREVA NA KATIBU MAHSUSI July 21, 2022
  • JOINING INSTRUCTIONS KWA SHULE ZA SEKONDARI ZA UBUNGO MANISPAA 2023. December 28, 2022
  • SELECTION ZA KIDATO CHA KWANZA UBUNGO MANISPAA 2023 December 28, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 02, 2022
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MAJALIWA AKAGUA MRADI WA KITUO CHA KIMATAIFA CHA KIBIASHARA MANISPAA YA UBUNGO

    April 20, 2023
  • WAZIRI KAIRUKI AWASILISHA BAJETI YA SHILINGI TRILIONI 9 KWA MWAKA WA FEDHA 2023/2024

    April 14, 2023
  • DC KOMBA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO UBUNGO

    March 31, 2023
  • MADIWANI UBUNGO WAPITISHWA KWENYE MAELEZO YA MPANGO KABAMBE (MASTER PLAN) WA MKOA WA DAR ES SALAAM

    March 28, 2023
  • Tazama zote

Video

BILIONI 1.4 KUJENGA VETA MPYA KIBAMBA | DC KOMBA ATOA SIKU 10 HATI YA ENEO IPATIKANE
More Videos

Viunganishi vya haraka

  • Leseni za biashara
  • Ushuru wa Hoteli
  • Kibali cha ujenzi
  • Sheria ndogondogo
  • Malengo na Dira
  • Muundo wa Uongozi
  • zabuni

Viunganishi linganifu

  • The National Examinations Council of Tanzania
  • TAMISEMI
  • Ministry of Education
  • President office State House
  • National Council for Technical Education
  • Ministry of Finace and Planning

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya wanaoingia

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Luguruni Area, Morogoro Road

    Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam

    Telephone: +255 22 2926341

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@ubungomc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa