Leo Wilaya ya Ubungo imepokea mapendekezo ya bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2020/2021 katika kikao maalum cha Kamati ya ushauri ya Wilaya.
Kikao hicho kimeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo *Mhe. Kisare Makori* ambae ndiye Mwenyekiti wa kikao, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic ambae ndie Katibu na Meneja wa TARURA Wilaya ya Ubungo Eng. Laynas Sanya ambae ndie aliyewasilisha bajeti hiyo.
Wengine waliohudhuria kikao hicho ni Wataalam wa Manispaa ya Ubungo na Viongozi wa vyama vya siasa, na watumishi wa TARURA.
Katika kikao hicho Meneja wa TARURA aliwasilisha bajeti ya matengenezo ya barabara ya kiasi cha Shilingi Bilioni 3.2 katika bajeti hiyo matengenezo ya kawaida ni Bilioni 1.8, sehemu korofi Milioni 404, matengenezo ya muda maalum Milioni 211 na ujenzi wa madaraja na calvert Milioni 635.
Mkuu wa Wilaya aliwaelezea wajumbe majukumu yao na kuwaambia umuhimu wa kikao. "Lengo la kikao ni kujiridhisha juu ya aina za barabara zilizotengewa fedha na kutoa ushauri, si hilo tuu kwa kuwa sisi tunazifahamu barabara zetu tunaweza kutoa mapendekezo na kuuliza maswali pia.
Katibu wa ACT Wilaya ya Ubungo alimpongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuitisha kikao na kusema kuwa kimekuwa na manufaa sana kwani wameweza kujua fedha zilizotengwa katika barabara za Wilaya ya Ubungo na wajumbe wameweza kujua majukumu yao.
Vile vile alimpongeza Meneja wa TARURA kwa uwasilishaji mzuri ambao umewafanya wajumbe wapate uelewa wa kutosha.
Wakati akifunga kikao Mkuu wa Wilaya aliwashukuru wajumbe kwa ujio wao na kuwaomba viongozi kuwa na uwajibikaji kwa maana ya kauli na vitendo na kuwa na staha.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa