MHESHIMIWA YUSUPH OMARI YENGA AIBUKA KINARA, PONGEZI NYINGI KWAKE
Manispaa ya Ubungo imepokea kwa bashasha matokeo ya uchaguzi wa Naibu Meya Manispaa ya Ubungo Mhe. YUSUPH OMARI YENGA kutoka Kata ya Mburahati ambaye ameshinda kwa kura 19 sawa na asilimia 95% nakupata nafasi ya kuwa Naibu Meya katika Manispaa hiyo akichukua nafasi ya aliyekuwa Naibu Meya Hassan Mwasha kutoka Kata ya Msigani
Uchaguzi huo umefanyika Leo agosti 15, 2022 ambapo Kila baada ya mwaka mmoja hufanyika uchaguzi kwaajili ya kumchagua Naibu Meya kwa mujibu wa Sheria.
Akitoa shukrani zake Mhe. YENGA ameshukuru wajumbe wa baraza hilo kwa kumpa kura za ndio
"Ntaenda kufanya kazi Kama mlivyonniamini , mnipe ushirikiano wenu" aliongeza Yenga
Nae aliyekuwa Naibu Meya Mhe. Hassan Mwasha ametoa shukrani zake za pekee katika baraza hilo kwa madiwani wote kwa ushirikiano mkubwa walio muonyesha kipindi alipokuwa Naibu na pia amempongeza Naibu Meya mpya kwa kupata nafasi hiyo
Aidha, katika baraza hilo wenyeviti na wajumbe wa kamati mbalimbali walichaguliwa
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James amempongeza kwa ushindi Naibu Meya YUSUPH OMARI YENGA na wajumbe wa kamati zote na kuwaahidi Serikali kuwapa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu
Nae Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ndugu, Beatrice Dominic amewapongeza wajumbe wa kamati zote na Naibu Meya kwa kuchaguliwa na kuahidi kuendelea kushirikiana bega kwa bega katika kutekeleza majukumu ya halmashauri
Halikadhalika, Zoezi la ugawaji wa vyeti vya shukrani kwa waliokuwa viongozi wa kamati zilizopita lilifanyika.
Pamoja na hayo baraza liliwapongeza mtendaji kata ya Ubungo, Mwenyekiti sinza C, mtendaji kata ya manzese, Mwenyekiti Mtaa wa kibangu na Mwenyekiti wa Msumi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa