Wajumbe kamati ya Mipango Miji Manispaa ya ubungo Leo tarehe 22 Julai, 2022 wametembelea kituo Cha uchakataji wa taka kilichopo Bonyokwa kinachojulikana Kama Material recovery facility center (MRF)
Katika ziara hiyo wajumbe waliweza kujifunza michakato mbalimbali inayotumika katika uzalishaji wa taka mpaka kufikia hatua ya uchakataji na namna taka hizo zinavyoweza kuleta manufaa kwa kupata kipato na hata kupunguza uchafuzi wa mazingira
Aidha walipongeza juhudi zilizotumika kwa waanzilishi wa kituo hicho kwa ubunifu waliofanya ambao unaenda kuleta manufaa makubwa ambapo mpaka sasa wanaendelea kutoa elimu kwa wengine kujifunza namna za uchakataji wa taka unavyofanyika
Pia kamati imetembelea eneo linalojengwa shule ya wasichana ya Mkoa lililopo Kwembe lenye ukubwa wa hekta 75 ambapo hekta 27 zinaenda kutumika kwaajili ya Ujenzi wa shule hiyo na kutoa mapendekezo yao kwaajili ya kufanya maboresho
Halikadhalika, Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bonyokwa ndgu. Maliyatabu Wakati amewakaribisha wajumbe kushiriki katika mafunzo pindi tu wanapohitaji kufahamu zaidi kuhusu elimu ya uchakataji wa taka
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa