Picha mbalimbali zikiwaonesha wajumbe wa Kamati ya mipango miji na mazingira wa Manispaa ya Ubungo wakiongozwa na mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Esther Ndoha Diwani wa Kata ya Goba, wakiwa kwenye ziara ya robo ya kwanza ya mwaka 2022/2023 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kutembelea eneo la viwanja vinavyomilikiwa na Manispaa hiyo lenye ukubwa wa ekari 11 lililopo Kata ya Kibamba Mtaa wa Gogoni.
Pamoja na kutembelea eneo hilo Kamati hiyo pia ilifanikiwa kutembelea eneo lililopo Kata ya Msigani Mtaa Msigani ambalo lilikuwa na mgogoro kati ya mzee Mtenga na wananchi wa Kata ya Msigani.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa