Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James amefanya ziara katika kata ya mbezi na kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kutatua kero za wananchi wa Kata hiyo
Akizungumza wakati wa ziara hiyo tarehe 20, septemba, 2021 Kheri amesisitiza wataalam,viongozi pamoja na walimu wa shule zilizotembelewa kuhakikisha utekelezaji wa miradi unafanyika kwa uweredi na ufanisi hasa kwa kuzingatia thamani ya fedha zinazotumika
Alipotembelea mradi wa ujenzi wa ofisi ya mwalimu mkuu Mbezi iliyojengwa kwa nguvu wananchi alisisitiza ukamilishwaji wa mradi huo kufanyika kwa haraka iliwananchi waweze kuona matunda ya jitihada zao
Aidha ametembelea mradi wa Madarasa mawili na Ofisi moja shule ya sekondari Mbezi inn,Ujenzi wa Barabara na daraja la Beda Amuri, kizimba Cha maji - kitope,ujenzi wa Madarasa 4 ,ofisi 1 na vyoo matundu 12 shule ya Msingi Makabe na utatuzi wa mgogoro wa uendeshaji stendi ya daladala Msumi baina ya madereva na wazawa
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa