Wajumbe wa Kamati ya Huduma za Uchumi ,Afya na Elimu Manispaa ya Ubungo wamefanya ziara ya kukagua miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika wilaya hiyo.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 15january,2022 nakutembelea Ujenzi wa Wodi ya wazazi katika Zahanati ya Mabibo iliyopo Kata ya Mabibo na ujenzi wa madarasa 8 katika shule ya sekondari Mabibo
aidha Wajumbe wamepongeza jitihada za serikali katika kihakikisha huduma zinawafikia wananchi wake kwani hatua ya miradi yote ipo hatua nzuri
sambamba na hayo Wajumbe hao wameagiza wodi ya wazazi katika zahanati ya Mabibo ianze kutumika kuanzia sasa ili huduma ziendelee kutolewa kwa wagonjwa wanaotaka kujifungua
ReplyForward |
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa