Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Kibamba ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa Jimbo la Kibamba Mh. Issa Jumanne Mtemvu Jumanne Machi 01, 2022 imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kupitia Mfuko huo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ikiwemo miradi ya elimu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 iliyogharimu Tsh Milioni 52,782,250/ =
Katika ziara hiyo Kamati imetembelea miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa utengenezaji wa viti na meza Shule ya Sekondari Goba, mradi wa mafunzo ya Sayansi Shule Sekondari Kibwegere unaojikita zaidi kwenye tafiti.
Baada ya ukaguzi wa miradi hiyo, Mbunge wa Jimbo la kibamba ambae ndiye mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Issa Mtemvu amesema kuwa Kwa kipindi cha mwaka mmoja Jimbo limepokea kiasi cha shilingi milioni 52,782,250/= kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayolenga hasa kutatua kero za Wananchi katika Nyanja mbalimbali za Maendeleo.
Na pia mtevu ameeleza kuwa katika kuwezesha wananchi kiuchumi ni vema wananchi wakachukua fursa ya kupata mikopo isiyo na riba inayotolewa na Manispaa kupitia asilimia 10 ya mapato yake ya ndani Kwa kijiunga kwenye vikundi ili wakopeshwe fedha hizo.
Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ni pamoja na Mradi wa ukarabati wa madarasa katika shule ya Msingi ya Mabake iliyopo Mbezi na Shule ya Msingi ya Abdul Wakil iliyopo Kibamba, mradi wa ununuzi wa mashine ya kusaga kwa kikundi cha wazee cha BAWAZI kilichopo Mbezi.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa