Kamati ya Fedha na Utawala Manispaa ya Ubungo imefanya ziara ya robo ya kwanza ya mwaka 2022/2023 Leo tarehe 10/11/2022 kwa kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo zahanati ya Kinzudi na eneo la viwanja vya Manispaa lenye ukubwa wa ekari 11.
Mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Kinzudi iliyopo Kata ya Goba mtaa wa Kinzudi umejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 121.6 ambazo ni fedha kutoka Serikali kuu na Fedha za mapato ya ndani ya Manispaa ambapo ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 95.
Pamoja na mradi huo Kamati ilitembelea eneo la viwanja vinavyomilikiwa na Manispaa hiyo lenye ukubwa wa ekari 11.
Akiongea katika ziara hiyo Mhe. Yusuph Yenga Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambae ni Kaimu Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo (Diwani wa Kata ya Mburahati) amesema ni vyema Manispaa kuendelea kufidia maeneo mengine mengi kwa ajili ya uwekezaji kwa maslahi ya wanaubungo.
“Haiwezekani kila eneo la Manispaa kuwa na makazi ya watu tu ni vyema kutenga maeneo mengine kwa ajili ya uwekezaji” Alisema Yenga
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa