Tarehe 25 Mei 2021 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi Dkt. Grace Maghembe amefanya ziara ya kutembelea mradi wa Hospitali ya Wilaya ya Ubungo iliyopo mtaa wa Baruti- kata ya Kimara na baada ya hapo akatembelea hospitali ya Sinza kwa lengo la kufuatilia utekeleza wa miradi inayotekelezwa na Halmashauri na kuona maendeleo yake
Katika ziara hiyo ameambatana na Mkurugenzi wa Afya Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka OR-Tamisemi Dkt. Ntuli Kapologwe wametembelea mradi wa hospital ya Wilaya ambao umeshapokea jumla ya fedha Tsh Billion 1.75 ambapo 1.5 billioni kutoka serikali kuu na milioni 250 kutoka katika mapato ya ndani lakini bajeti ya awali ya mradi ulikadiriwa kukamilika kwa gharama ya fedha jumla Tshs 1,826,811,290.10 .
Dk.Grace mpongeza Mkurugenzi pamoja na watalaam kwa utekelezaji wa mradi huo uliozingatia viwango vinavyostahili
"tutawalete watumishi 10 waongeze nguvu katika idara ya afya na fedha million 800 kwaajili ya ujenzi wa jengo la wodi, mochwali na jengo la upasuaji" Alisema hayo Dkt.Grace
Aidha wakati wa akiwasilisha taarifa kuhusiana na mradi huo Mganga mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt.Peter Nsanya alieleza kuwa mpaka sasa mradi huo umekamilika kwa 90% ukihusisha majengo saba (Jengo la wagonjwa wa nje ,jengo la wazazi,jengo la kufulia,utawala,Stoo ya Dawa ,Maabara na Jengo la wazazi)
Sambamba na hayo Dkt. Grace aliwaagiza wataalam kuzingatia mifumo mizuri ya kushughulikia wananchi kero zao na aliwakuta wana kikao cha Kamati ya fedha chanHalmashaui nankuwataka madiwani kuhakikisha wanasimamia swala zima la ukusanyaji wa mapato na matumizi ya halmashauri
Na pia utunzaji bora mazingira kwa afya ya wanachi wa ubungo na kuepukana na magonjwa ya milipuko
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa