Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Jaffary Juma Nyaigesha ametembelewa na Naibu Mstahiki Meya wa Mjini Zanzibar Khadija Miraji lengo likiwa ni kujifunza namna Bora ya usimamizi wa miradi, ukusanyaji wa Mapato na udhibiti wa matumizi na hali inayowafanya kupata hati Safi katika ukaguzi wa hesabu za Serikali.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo amepokea wageni hao leo Mei 31, 2021 ambapo watajifunza mambo mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa Mapato na matumizi ya Fedha kwa ajili ya maendeleo kwa wananchi wake na kutembelea mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya na Kituo cha mabasi ya Magufuli
Akiongea wakati wa kuwakaribisha wageni hao Nyaigesha alisema kuwa, ni heshima kubwa kwa Manispaa hiyo kutembelewa na ugeni huo imesaidia katika kuboresha mahusiano na mwanzo mzuri wa kuhakikisha wanajenga mahusiano yaliyo bora
Aidha kiongea wakati wa kikao hicho Mkurugenzi wa manispaa ya ubungo Beatrice Dominic alifafanua namna ambavyo halmashauri inafanya matumizi kutokana na mapato inayokusanywa
Beatrice alieleza kuwa asilimia 60% ya mapato yanayokusanywa ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na 40℅ kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya Halmashauri
Beatrice aliendelea kusema kuwa Halmashauri hukusanya mapato yake kutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo ulipishaji wa ada za leseni za biashara, ushuru wa huduma, leseni za vileo, na tozo mbalimbali za Halmashauri ambapo mpaka sasa Manispaa imekusanya Billioni 16.413 Sawa na 91% ya makusanyo na hadi kufikia June 30 asilimia iliyobaki itakuwa imekusanywa ili kukamilisha asilimia 100 ya mapato yake.
Pia Manispaa ya ubungo kwa kipindi cha miaka minne mfululizo imefanikiwa kupata hati Safi katika kaguzi za hesabu za serikali na Manispaa itaedelea kusimamia kanuni, sheria na miongozo ya makusanyo na matumizi ya Fedha za Umma ili kuendelea kupata hati Safi
Nae Khadija Miraji aliipongeza manispaa ya ubungo kwa utekelezaji wa miradi na utendaji wake katika swala zima la ukusanya wa mapato na matumizi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa