Naibu waziri wa Nishati Mhe. SUBIRA MGALU ametembelea Wilaya ya Ubungo na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.KISARE MAKORI na Mbunge wa Kibamba Mhe.JOHN MNYIKA pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Kilimo Bi.HAPPINESS MBELLE wakati wakitembelea miradi mbalimbali ya umeme iliyopo Wilayani Ubungo. Katika ziara hiyo miradi iliyotembelewa ni mradi wa umeme wa Kibesa uliopo kata ya Mbezi, mradi wa Derlini uliopo kata ya Kibamba, King'azi uliopo kata ya Kwembe, Msumi uliopo kata ya Mbezi. apata malalamiko ya wananchi wa kibamba umeme umekua ukikatika mara kwa mara ni agize TANESCO muhakikishe mnazingatia ilo sitaki kusikia tena malalamiko aya kwa watu wa Kibamba"* alisema Naibu Waziri Mpaka ifikapo disemba kama mlivyonihakikishia muwe mumetimiza ahadi yenu, maeneo yote ya Kibesa na sehemu ambazo mmehaidi kutimiza kazi yenu iwe ipasavyo, mpaka krismas watu hawa wawe wamepatiwa umeme katika maeneo yao.
Naomba niagize ifikapo muda mlioniahidi ntafika apa na dhumuni langu ni kukaa na watu hawa na kusherekea nao wakiwa wanatumia umeme katika nyumba zao, agizo la Mhe.Rais ni kuhakikisha Watanzania hawa wanaishi katika mazingira mazuri na umeme ni moja ya nishati inayotumika kwa kila mtu katika majumba yetu na kwa kuhakikisha ilo muweke umeme katika maeneo yote tuliyopita na mmehaidi mtawawekea umeme mpaka ifikapo disemba, isiwe kinyume na ahadi mliyotoa. alisema Waziri wakati akitoa maagizo kwa wafanya kazi wa TANESCO. Nina washa umeme apa leo naomba nisisikie kuwa umeme unakatikakatika iwe mfano alisema ayo Mhe. Naibu Waziri *Wakati akitembelea eneo la Msumi B na kufanya uzinduzi wa nyumba ambayo imeingizwa umeme* ni moja ya nyumba ya mwanachama wa saccos ndg. Shirima anayeishi eneo la Msumi B.
Nae Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe.Kisare Makori ameshukuru ujio wa Mhe.Naibu Waziri katika Wilaya Ubungo kwani umekuja kutatua changamoto wanazozipata watu na kushukuru kwa *Mhe.Rais Dr.JOHN POMBE MAGUFULI* kwa uongozi wake wa awamu ya tano wenye kasi ya kufanya kazi na viongozi kujituma ipasavyo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa