Mganga Mkuu Manispaa ya Ubungo Dk.Peter Nsanya aendesha zoezi la upuliziaji dawa lililofanyika tarehe 30/3/2020 akiongozana na Mratibu wa zoezi la unyunyuziaji wa dawa Dk.Ford Chisongela na wataalam kutoka Idara ya afya.
"Uendeshaji wa zoezi hilo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa PAUL MAKONDA la upuliziaji wa dawa kwaajili ya kuuwa vijijidudu vyote vinavyosababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo na vijijidudu vya Korona
Aidha zoezi hilo limefanyika stendi kuu ya mabasi Ubungo na kupita pembezoni mwa barabara ya Sinza,Ubungo na Shekilango.
Katika kufanikisha tukio hilo magari matatu yalitumika ambalo moja ni kutoka kitengo cha zima Moto lenye ujazo wa lita18000, gari la police ujazo wa lita 6000, na gari moja kutoka ofisi ya Mkurugenzi lililobeba fogging machine kwa ajili ya kuuwa mbu wa aina zote.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa