Malengo na majukumu ya idara ya elimu msingi.
Kazi kubwa ya Idara ya Elimu Msingi ni kama ifuatavyo-:
Ø Kuongeza uandikishaji kwa kuzingatia fursa sawa.
Ø Kuinua ubora wa Elimu katika ngazi zote kwa Halmashauri.
Ø Kusimamia uwezo wa utendaji kazi.
Ø Kushughulikia masuala ya mtambuka na taratibu za kitaasisi.
Ø Kufanya utafiti wa Kielimu,ufuatiliaji na tathmini za Kielelimu.
Ø Kupunguza idadi ya watu wazima wasiojua kusoma na kuandika
Ø Kuinua ubora wa mazingira ya Kufundishia na kujifunzia wanafunzi wote.
Ø Kuongeza idadi ya madarasa na watoto wa shule za awali.
Ø Kuhakikisha kuwa Elimu ya UKIMWI (VVU), Mazingira na stadi za maisha zinatolewa kwa ufanisi katika shule za msingi.
Ø Kusimamia upatikanaji na uwezeshaji wa mazingira kwa wanafunzi wenye Ulemavu.
Mikakati iliyopo ili kuboresha elimu na kuinua kiwango cha taaluma na kufanikisha mpango wa Matokeo Makubwa Sasa.(BRN).
Kutekeleza shughuli muhimu kulingana na ufinyu wa bajeti uliopo.
Kuboresha Taaluma kwa kugawa maafisa Elimu kila kata kwa ajili ya ufuatiliaji wa karibu wa Taaluma na matatizo ya walimu.
Kuboresha miundo mbinu na mazingira ya kujifunza na kujifunzia kwa kutumia fursa zilizopo.
Kufanya vikao mbalimbali vya kila mwezi kati ya Maofisa Elimu, Waratibu na Walimu Wakuu kwa kuzingatia ratiba maalum iliyoandaliwa.Vikao rasmi Vinne kila mwezi vimekwishafanyika kufikia sasa.
Uendeshaji wa Semina mbalimbali za masomo na semina za kitaalamu na kufanya mrejesho shuleni.
Kuwajengea uwezo Kamati za Taaluma kwa kila shule ili kuweza kufanya upimaji na tathimini kupata mweleko wa Maendeleo ya Wanafunzi.
Kuimarisha Vyama (Clubs) za masomo na k.k.k mashuleni .
Kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. Mfano Wazazi, watu binafsi na mashirika mbalimbal na Makampuni.
Shughuli za Elimu ya Watu wazima-
Kitengo hiki kinatekeleza shughuli zifuatazo-:
Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Waliokosa(MEMKWA)
Mpango wa Uwiano kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii(MUKEJA)
Program ya Elimu ya Sekondari Huria (PESH)
Elimu Masafa na Ana kwa Ana(ODL)
Program ya Ndiyo Ninaweza(YES I CAN)(Idadi ya vituo vimeambatanishwa)
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa