MIPANGO MIJI, ARDHI
Idara ya Mipangomiji na Ardhi hushughulikia masuala mbalimbali kuhusu uendelezaji wa Makazi, Ardhi na Maliasili. Idara hii inatekeleza na kusimamia Program mbalimbali zinazohusiana na maendeleo ya makazi ikiwemo Program ya kuboresha miundombiu ya jamii katika maeneo yasiyopangwa (DMDP), Program ya Mtandao wa Miji Tanzania (TACINE).
Muundo wa Idara
Idara ya Mipangomiji na Ardhi ni mojawapo kati ya Idara 19 za Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo zinazofanya kazi chini ya Mkurugenzi wa Manispaa. Idara imegawanyika katika sehemu nne zinazojumuisha Miliki na Maendeleo ya ardhi, Mipango ya Makazi, Uthamini, Upimaji na Ramani
Majukumu ya Idara
Kuandaa na kusimamia utekelezaji mipango ya uendelezaji wa ardhi katika Manispaa kwa kuzingatia Mpango Kabambe, Sheria ya Mipangomiji Sura Na. 8 ya mwaka 2007, sheria ya Ardhi na 4 ya mwaka 1999 na kanuzi zake pamoja na mingozo mingine inayotolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Ø Upimaji wa viwanja vya matumizi mbalimbali
Ø Uthamini wa majengo na mazao kwa ajili ya fidia, kodi ya majengo, mauzo, rehani na huduma nyinginezo.
Ø Kuchunguza ramani za ujenzi zinazowasilishwa kwa ajili ya maombi ya vibali vya ujenzi.
Ø Kuchunguza na kupitisha fomu za maombi ya leseni za biashara mbalimbali.
Ø Kusimamia utunzaji, kuhifadhi, kuimarisha na kuendeleza rasilimali ya maliasili.
Ø Kuandaa miliki za viwanja mbalimbali
Ø Kusimamia utekelezaji wa program zifuatazo:-
i. Mradi wa kuboresha miundo mbinu kwenye maeneo yasipangwa (DMDP)
ii. Usimamiaji na utunzaji wa takwimu za kijiografia (GIS)
iii. Kutambua na kutoa haki miliki katika maeneo yasiyopimwa (Leseni za Makazi)
iv. Kuratibu Program ya Mtandao wa Miji Tanzania (TACINE)
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa