MADHUMUNI YA MTANDAO:
. Mtandao huu utawaunganisha wafugaji wote wa n’gombe na mbuzi wa maziwa wa katka
Manispaa yote ya Ubungo, wakiwemo wafugaji wadogo, wa kati na wakubwa.
. Utatumika kama baraza la kubadilishana taarifa baina ya wadau wa tasinia ya maziwa
kwa mambo mbali mbali yakiwemo bei za maziwa, bei za mifugo, milipuko ya
magonjwa ya mifugo, wizi wa mifugo nk.
. Kutambua matatizo ya tasinia ya maziwa na kupeleka mapendekezo serikalini ili kupata
ufumbuzi wa pamoja.
. Kutoa elimu na hamasa ya ufugaji mjini kwa kufuata sheria za ufugaji bora bila ya
kuharibu mazingira na kuleta kero kwa jamii.
. Kutoa elimu ya jinsi ya kuongeza mnyororo wa thamani katika zao la maziwa.
. Kushirikisha wadau wengine wakiwemo wafugaji, mafiasa ugani, watafiti, watunga sera
na mashirika yasiyo ya kiserikali mfano, World vision, Heifer Project Tanzania, Farm
Africa nk.
. Kushirikiana katika matumizi bora ya rasilimali(watu, fedha, vifaa, miundo mbinu na
kubadilishana wanyama) ili kuepuka mifugo kuzaliana ndugu wa karibu (In breeding)
. Kuanzisha vituo vya uhamilishaji kwa njia ya mirija (AI) na vituo vya kukusanyia
maziwa(Milk collection centers) kwa kuyatumia mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na
wadau wengine waliotayari kuwekeza katika tasinia ya maziwa.
. Kushirikiana na mitandao mingine inayojishughulisha na tasinia ya mifugo ndani na nje
ya nchi.
. Kuhamasisha uanzishaji wa Saccos, Vicoba, na maduka ya pembejeo za mifugo katika
jamii zetu ili kurahisisha upatikanaji wa huduma.
. MATARAJIO YA BAADAE:
. Wadau wote watanufaika na huduma bora mbali mbali za utaalam wa kisasa katika
tasinia ya maziwa vikiwemo kuhudhuria maonesho ya nane nane, ziara za mafunzo,
kupata elimu ya ujenzi wa mabanda bora na utunzaji sahihi wa kumbukumbu za miradi
yao.
. Kuongeza ubora wa mziwa kwa kuyachakata na kuzalisha mazao mengine yatokanayo na
maziwa mf. Jibini, maziwa lala, samli nk.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa