Kutokana na mgao wa fedha zilizotokana na Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 Manispaa ya Ubungo ni miongozi mwa Manispaa zilizonufaika na mgao huo ambapo ilipata Tsh Bilioni 3.02 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa madarasa 151 katika shule 21 zilizopo Manispa hiyo na kati ya hizo zimejengwa shule mpya mbili za sekondari.Asante Mhe. Rais wa awamu ya sita, kaziiendelee.
Kikundi hiki kinapatikana Wilaya ya Ubungo Kata ya Kibamba ambapo kinajihusisha na utengenezaji wa mapambo ya mikanda ya gypsum kwa sasa lakini kinamatarajio makubwa yakutengeneza mapambo yote yanayotokana na gypsum ambapo kwa sasa kinasubiri kuingiziwa fedha za mkopo wa 10% ya mapato ya ndani ya Manispaa kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambapo kikundi cha vijana hao kitaingiziwa fedha hizo kwa ajili ya kukuza biashara yao.
Kamati ya siasa Mkoa walipotembelea utekelezaji wa miradi ya maendeleo Manispaa ya Ubungo na kufurahishwa jinsi Manispaa inavyotekeleza miradi hiyo.
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa